Matthew 18:1-5

Aliye Mkuu Katika Ufalme Wa Mbinguni

(Marko 9:33-37; Luka 9:46-48)

1 aWakati huo, wanafunzi wakamjia Yesu na kumuuliza, “Je, nani aliye mkuu kuliko wote katika Ufalme wa Mbinguni?”

2Yesu akamwita mtoto mdogo na kumsimamisha katikati yao. 3 bNaye akasema: “Amin, nawaambia, msipookoka na kuwa kama watoto wadogo, kamwe hamtaingia katika Ufalme wa Mbinguni. 4 cKwa hiyo mtu yeyote anyenyekeaye kama huyu mtoto, ndiye aliye mkuu kuliko wote katika Ufalme wa Mbinguni.

5 d “Yeyote amkaribishaye mtoto mdogo kama huyu kwa Jina langu, anikaribisha mimi.
Copyright information for SwhNEN